🚨 𝐁𝐑𝐄𝐀𝐊𝐈𝐍𝐆: 𝐒𝐈𝐌𝐁𝐀 𝐒𝐂 𝐈𝐓𝐀𝐂𝐇𝐄𝐙𝐀 𝐍𝐀 𝐓𝐔𝐒𝐊𝐄𝐑 𝐅𝐂 𝐘𝐀 𝐊𝐄𝐍𝐘𝐀 𝐊𝐖𝐄𝐍𝐘𝐄 𝐒𝐈𝐌𝐁𝐀𝐃𝐀𝐘 𝟐𝟎𝟐𝟔! 😍🦁 Simba SC 🇹🇿 rasmi itacheza dhidi ya Tusker 🇰🇪 kwenye sherehe za SimbaDay 2026 na mchezo huo wa kimataifa wa kirafiki utachezwa tarehe 08-08-2026 katika uwanja wa Uhuru. 🔚 Awali Simba walituma ombi la kuialika FC Dynamos ya Zimbabwe 🇿🇼 lakini mpaka sasa klabu hiyo ya Zimbabwe haijatoa majibu na ndipo Simba SC ikabadili maamuzi ya kuialika Tusker ya nchini Kenya ambayo imejibu kwa wakati na kukubali kushiriki mchezo huo. WACHEZAJI WAPYA SIMBA MPAKA SASA : 🇿🇦 Keletso Makgalwa – ametokea Sekhukhune United (Afrika Kusini). 🇮🇶 Ibraheem Jabaar – ametokea Stellenbosch FC (Afrika Kusini). 🇨🇮 Serge Badjo – ametokea USM Alger (Algeria). 🇹🇿 Kelvin Nashon – ametokea Pamba Jiji FC (Tanzania). 🇹🇿 Bakari Msimu – ametokea Coastal Union (Tanzania).
ADVERTISEMENT